Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora SMZ Mhe. Dk. Mwalimu Haroun Ali Suleiman akizungumza mbele ya wawakilishi wa Asasi za kirai 14 za kisiwani Zanzibar wakati akifungua kikao kazi cha kupitia rasimu ya taarifa ya Nchi ya utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na itifaki ya Haki za wanawake Afrika Machi 26, 2025.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Haki za Binadamu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Beatrice Mpembo akizungumza mbele ya wawakilishi wa Asasi za kirai 14 za kisiwani Zanzibar wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kupitia rasimu ya taarifa ya Nchi ya utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na Itifaki ya Haki za Wanawake Afrika Machi 26, 2025 Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora SMZ Mhe. Dk. Mwalimu Haroun Ali Suleiman (Wanne Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria na Watumishi wa Wizara anayoingoza baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha kupitia rasimu ya taarifa ya Nchi ya utekelezaji wa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu pamoja na itifaki ya Haki za Wanawake Afrika Machi 26, 2025 Zanzibar.
Baadhi ya Wakurugenzi na Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula wakiwa katika picha ya utayari wa kushiriki katika mazoezi ya kwa ajili ya kuimarisha afya zao wawapo kazini. 25 Machi, 2025.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula akimkabidhi Bi. Rhoda Longwe fulana na vifaa vya mazoezi kwa niaba ya Watumishi wa Wizara ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha Watumishi hao wanapata vifaa kwa ajili ya kushiriki katika mazoezi ya mwili kwa siku za Jumanne na Alhamisi ikiwa ni kuimarisha afya zao wawapo kazini. Tarehe 25 Machi, 2025.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg.Eliakim Maswi akiwasilisha Randama ya Mpango wa Bajeti ya mafungu yaliyopo chini ya Wizara kwa mwaka 2025/26 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria tarehe 24 Machi, 2025 Bungeni jijini Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara kwa lengo la kupitia bajeti kwa kipindi cha mwaka 2025/26 za mafungu yaliyo chini ya Wizara. Machi 23, 2025 Mtumba, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Maswi akizungumza wakati wa uwasilishaji wa mapendekezo ya rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2025/26 kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ikiwa ni maandalizi ya kuiwasilisha mbele ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Bungeni, jijini Dodoma. Machi 23, 2025 Mtumba, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Rwezimula akiweka nukuu ya mambo muhimu wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya mapendekezo ya rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2025/26 kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ikiwa ni maandalizi ya kuiwasilisha mbele ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Bungeni, jijini Dodoma. Machi 23, 2025 Mtumba, jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara wakiwa pamoja na Maafisa Bajeti wakipitia taarifa za uwasilishaji wa mapendekezo ya rasimu ya Bajeti kwa mwaka 2025/26 kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ikiwa ni maandalizi ya kuiwasilisha mbele ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Bungeni, jijini Dodoma. Machi 23, 2025 Mtumba, jijini Dodoma.