• MIAKA 50 MUUNGANO
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kisheria kwa Umma Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Felistas Mushi.
 • KATIBU MKUU-MOCLA
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde (kulia) akimhudumia mwananchi aliyefika katika banda la Wizara yake kupata taarifa mbalimbali.
 • BAJETI
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Asha Rozi Migiro (MB)wa Wizara ya Katiba na Sheria akifanunua jambo wakati wa mkutano na watendaji wakuu wa taasisi zilizo chini ya wizara wa makadirio ya fedha za matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo uliofanyika jana (29/04/2014) katika ukumbi wa Wizara.
 • BARAZA
  Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika jijini Dar-es-salaam (Jumatano, April,2014)
 • TUGHE
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar es salaam Bw. Hassan Kaumo akiongea na wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo jijini Dar es salaam uliofanyika Jumatano April30,2014. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Fanuel Mbonde.
 • WATUMISHI-SHERIA
  Bi. Flora Fissoo (Kulia), Bi.Agnes Tumbuchile (Katikati) na Bi. Rahma Ubuguyu, wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika jijini Dar-es-salaam (Jumatano, April,2014)
 • DK.MIGIRO
  Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha Rozi Migiro akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2014/2015 mbele ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria katika kikao kilichofanyka hivi karibuni jijini Dar es salaam.
 • KAIRUKI UNDP
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki akiagana na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) Bi. Mandisa Mashologu (kulia) alipomtembelea Naibu Waziri ofisini kwake, Mtaa wa Mkwepu, jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Mei 19, 2014). Katikati ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bw. Philippe Poinsot.
 • Dkt. Migiro
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Asha- Rose Migiro akipokea Taarifa juu ya Mapitio ya Mfumo wa Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe Jaji Aloysius Mujulizi Dodoma Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume Bi. Winfrida Korosso.
 • KM
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Fanuel Mbonde akifungua mafunzo kuhusu uzingatiwaji na uelewa wa masuala ya Jinsia kwa watumishi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 • JAJI
  Mkufunzi wa Masuala ya Jinsia na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Nchini (TAWJA) Jaji Engera Mmari Kileo akiongea wakati wa mafunzo kuhusu uzingatiwaji na uelewa wa masuala ya jinsia kwa watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria jijini Dar es Salaam mwishoni mwaka wiki.
 • EMMANUEL BARIGILA
  Bw. Emmanuel Barigila Afisa Uchunguzi kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRGG)akitoa mada kuhusu uzingatiaji wa Haki za Binadamu katika ofisi za umma kwa wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na wasaidizi wao (hawapo pichani)katika ukumbi wa mikutano Wizarani.
 • MENEJIMENTI
  Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wasaidizi wao wakisikiliza mada ya Utekelezaji wa majukumu Serikalini na Ufinyu wa Bajeti iliyotolewa na Mtaalam wa Mawasiliano Serikalini Dk. Henry Mambo (hayupo pichani) kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika ukumbi wa mikutano Wizarani.

Habari Mpya

Viongozi

Upo Hapa: Home

Wizara ya Katiba na Sheria ilianzishwa kwa tamko la Rais toleo Na.20 la mwaka 2008. Wizara hii ndiyo mhimili Mkuu wa Serikali katika masuala yote ya Kisheria katika nchi. Jukumu la msingi la Wizara ni kuhakikisha kuwa kuna utawala wa Sheria unaozingatia Katiba ya nchi.

Aidha, ni jukumu la Wizara, kuona kwamba Serikali na Taasisi zake zinasimamia Sheria kwa ufanisi na kwa dhati na kuwa wananchi wanapaswa kufuata na kuheshimu Sheria. Kwa ujumla Wizara inalo jukumu la kuhakikisha  kunakuwepo mfumo wa Sheria unaotoa fursa sawa kwa watu wote katika jamii ili kuweza kuendesha shughuli zao kwa ufanisi kwa ajili ya maendeleo yaTaifa.

 

dhamira
dira
dhamira
dira