• kadi
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
 • Waziri Kabudi awasili Dodoma
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma.
 • Kabudi
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
 • balozi korea
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Bw. Song, Geum-young alipomtembelea ofisini kwake mapema leo (17/11/2016) jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Msaidizi wa Balozi Bw. Song Wong (kulia) na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Abdala Kirumbu (kushoto).
 • felistas
  Mtanzania Felistas Joseph, amechaguliwa kuongoza Kamati ya nchi za Maziwa Makuu ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari (International Conference on Great Lakes Region –ICGLR).
 • koreaa
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiwaonesha Balozi wa Serikali ya Jamhuri ya Korea Bw. Song, Geum-young na Msaidizi wake Bw. Song Wong ramani ya Mkoa wa Mbeya na kuwakaribisha kutembelea vivutio vya Mkoa huo ikiwemo Ziwa Nyasa.
 • upr
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.
 • uprr
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango (kulia) alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Katiba Bw. Stanley Kamana.
 • Waziri Mwakyembe atembelewa na Balozi wa Uturuki
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Mhe Yasemin Eralp alipomtembelea ofisini kwake leo (16/11/2016) jijini Dar Es Salaam.
 • balozi india
  Balozi wa India nchini Tanzania Mh. Sandeep Arya akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe alipomtembelea ofisini kwake leo (15/11/2016) jijini Dar Es Salaam.
 • Balozi Jaap
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akibadilishana mawazo na Balozi wa Uholanzi Bw. Jaap Fredericks kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria ofisini kwake leo tar.20/09/2016.
 • Balozi Korea
  Katibu Mkuu Pro. Sifuni Mchome wa Wizara ya Katiba na Sheria akiongea na Balozi wa Korea nchini Tanzania kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya Sheria.
 • Mwakyembe
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe atembelewa na Jaji Mkuu wa Australia Kusini Bw. Christopher Kourakis ofisini kwake jijini Dar es salaam.
 • Balozi Christopher
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika ya pamoja na Balozi wa Australia Kusini (wa pili kulia)baada ya mazungumzo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar es Salaam.
 • Balozi Christopher
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akiwa katika ya pamoja na Balozi wa Australia Kusini (wa pili kulia)baada ya mazungumzo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar es Salaam.
 • Mwakyembe
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara athari za suala la ushoga na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.
 • Mwakyembe
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akisoma katika ukumbi wa mikutano wa Wizara moja ya nyaraka ambazo zinatumiwa na asasi za kiraia zinazojihusisha na masuala ya ushoga nchini.
 • Washiriki Ndoa
  Mshiriki wa Kikao kazi Bw.Japhace Daudi akiwasilisha baadhi ya marekebisho yaliyofanyiwa kazi kwa washiriki ya Sheria ya Ndoa 1971 katika ukumbi wa maktaba Law School jijini Dar Es Salaam.
 • Mama Mushi
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma Sehemu ya Msaada wa Sheria Bi. Felistas Mushi akiongea na washiriki wa kikao kazi cha marekebisho ya Sheria ya ndoa namna ya kufanya kazi hiyo katika moja ya darasa la Law School jijini Dar Es Salaam ambapo kazi hiyo ilifanyika.
 • Washiriki-Sheria ya ndoa 1971
  Washiriki wa Kikao cha Kazi cha marekebisho ya Sheria ya ndoa 1971 wakiandika mapendekezo yaliyotolewa na moja ya kikundi katika ukumbi wa makataba jijini Dar Es salaam.

Habari Mpya

Viongozi

Upo Hapa: Home

WATUMISHI WA SHERIA WAASWA

WATUMISHI WA SHERIA WAASWA KUCHAPA KAZI

Na Martha Komba

Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo lililofanyika leo (Alhamisi April 30, 2014) katika ukumbi wa Wizara jijini Dar-es-salaam.

“Uwajibikaji ni suala muhimu sana katika utumishi wa umma,” alisema katika mkutano huo wa siku moja uliofanyika jijini Dar-es-salaam.

Awali akiongea katika mkutano huo Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutimiza wajibu wao katika sehemu zao za kazi.

“Wafikishieni salamu hizi wafanyakazi wote, wachape kazi ili kuwapa viongozi nguvu ya kudai maslahi bora,” alisema.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine, ulijadili maslahi ya watumishi na kupitia Taarifa ya Mpango wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka ujao wa fedha 2014/2015.

Matukio Mapya

Hakuna Tukio kwa sasa.

Anuani

KATIBU MKUU

 • Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria,
 • Barabara ya Mkalama,
 • Jengo la Taaluma Na. 1,
 • Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM,
 • S.L.B. 315,
 • DODOMA.
 • Simu:+255 26 2321680
 • Nukushi: +255 26 2321679
 • Tovuti www.sheria.go.tz
 • Barua pepe: km@sheria.go.tz