• mkaguzi
  Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya katiba na Sheria Bibi Leticia Nchwali akiongoza kikao cha Wakaguzi wa Ndani wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara kuhusu hoja mbalimbali kutoka kwa CAG. Kikao hicho Kilifanyika jana (19/03/2014) katika ukumbi wa Wizara ya Katiba na Sheria.
 • cag
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wakaguzi Wakuu wa Ndani kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria wakijadili hoja mbalimbali kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali.
 • mkaguzii
  Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Melton Nyela(katikati) ambaye ni mwalikwa katika Mkutano wa wakaguzi wa ndani wa Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zilizo chini yake akichangia mawazo yake katika kujadili hoja za CAG.
 • wanawake
  Watumishi wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke jijini Dar Es Salaam. Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 08/03/2014.
 • WANAWAK
  Watumishi wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani)huku wakinyanyua kofia juu katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani iliyoadhimishwa tarehe 08/03/2014 katika viwanja vya Mwembeyanga Jijini Dar es Salaam.
 • lrc ziara
  Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro (aliyesimama)akiongea na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (hawapo pichani) wakati wa ziara yake katika Tume hiyo. Aliyeko kulia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki na aliyeko kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mh. Jaji Aloysius Mujulizi.
 • lrc ziaraa
  Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro (kushoto) akipokea taarifa mbalimbali zilizoandaliwa na Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Anayemkabidhi taarifa hizo ni Katibu wa Tume hiyo Bibi Winnie Korosso. Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki.
 • lrc ziar
  Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Aloysius Mujulizi(aliyesimama) akitoa taarifa fupi ya Tume hiyo kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro(waliokaa mbele katikati) wakati wa ziara ya Mh. Migiro katika Tume hiyo. Kushoto kwa Waziri Migiro ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki. Wengine ni Viongozi na watumishi wa Wizara na Tume ya kurekebisha Sheria.
 • mahakam
  Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman alipomtembelea ofisini kwake kwa mara ya kwanza leo (28/1/2014)tangu alipoteuliwa kuongoza Wizara hiyo.
 • mahakama
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman akifafanua jambo kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro (katikati)leo (28/1/2014) asubuhi wakati Mh. Migiro alipomtembelea ofisini kwake. Aliyeko kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki.
 • mahakamaa
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde (wa kwanza kulia) na viongozi mbalimbali wa Wizara na Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro(hayupo pichani) alipomtembelea Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani) ofisini kwake mapema leo (28/1/2014).
 • ziara
  waziri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro (kushoto) akiongea na watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (hawapo pichani) alipotembelea ofisi hizo jana (27/1/2014). Aliyeko kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki.
 • ziara waziri
  Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Asha Rose Migiro akiteta na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju wakati wa ziara yake katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali jana (27/1/2014).
 • ziara agc
  Mkurugenzi wa mashtaka nchini Bw. Eliezer Feleshi (kushoto)akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde (katikati)na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Msaada wa Kisheria Wizara ya Katiba na Sheria Bw. John Rwabuhanga wakati wa ziara ya Waziri wa Katiba na Sheria (hayupo pichani) katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 • waziri kikao
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Asha-Rose Migiro akiongea na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara hiyo (hawapo pichani) mara baada ya kumpokea Wizarani hapo. Aliyeko kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg. Fanuel Mbonde.
 • mapokezii
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Asha Rose Migiro (mwenye miwani) akiingia Wizara ya Katiba na Sheria baada ya kuapishwa kuiongoza Wizara hiyo na kupokewa na wafanyakazi wa Wizarani hapo.
 • mapokezi
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Fanuel Mbonde (kushoto) akimpokea Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Asha-Rose Migiro aliporipoti ofisini baada ya kuapishwa kuiongoza Wizara hiyo.
 • kiapo
  Mhe. Asha-Rose Migiro akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
 • familia
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na familia ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Asha-Rose Migiro baada ya kuapisha Mawaziri tarehe 21/01/2014.

Habari Mpya

Viongozi

Upo Hapa: Home

Wizara ya Katiba na Sheria ilianzishwa kwa tamko la Rais toleo Na.20 la mwaka 2008. Wizara hii ndiyo mhimili Mkuu wa Serikali katika masuala yote ya Kisheria katika nchi. Jukumu la msingi la Wizara ni kuhakikisha kuwa kuna utawala wa Sheria unaozingatia Katiba ya nchi.

Aidha, ni jukumu la Wizara, kuona kwamba Serikali na Taasisi zake zinasimamia Sheria kwa ufanisi na kwa dhati na kuwa wananchi wanapaswa kufuata na kuheshimu Sheria. Kwa ujumla Wizara inalo jukumu la kuhakikisha  kunakuwepo mfumo wa Sheria unaotoa fursa sawa kwa watu wote katika jamii ili kuweza kuendesha shughuli zao kwa ufanisi kwa ajili ya maendeleo yaTaifa.

 

dhamira
dira
dhamira
dira