Uzinduzi rasmi wa Kitaifa wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili (MSLAC II) unatarajiwa kufanyika 20 Juni, 2026, Dole-Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo mara baada ya kufungua rasmi mafunzo ya kulinda, kukuza na kutetea haki za watu wenye ulemavu, 8 Juni, 2026, Morena, Jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele (Katikati), katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama wa Waandishi wa Habari Wilaya ya Tarime baada ya kufungua rasmi Mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu upatikanaji haki kupitia huduma za msaada wa kisheria, 8 Juni, 2026, Tarime.
Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Athumani Msosole akitoa elimu ya Msaada wa Kisheria kwa waandishi wa habari kutoka katika Wilaya ya Tarime, 8 Juni, 2026.
Siku ya Mazingira Duniani tarehe 05 Juni, 2026
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. John Jingu, akiwa pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza, Jeremia Katundu mara baada ya kukamilika kwa kikao cha majadiliano ya kuimarisha ushirikiano katika utoaji wa huduma za Msaada wa Kisheria Magerezani.Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 03 Juni, 2026 Mtumba jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki Jane Lyimo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wataalamu kutoka Taasisi za mnyororo wa Haki Jinai kujadili maendeleo ya Mfumo wa National Legal Information System (NALIS).Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Wizara Mtumba Jijini Dodoma, tarehe 03 Juni, 2026
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Nkasori Sarakikya akimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria wakati wa uzinduzi wa Bustani ya Miti iliyoanzishwaa mwaka 2022 Nkuhungu jijini Dodoma, kwa lengo la kuimarisha uhifadhi wa mazingira,kukuza ustawi wa jamii na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Zainab Katimba (Kushoto) akikabidhi tuzo ya Shukran kwa Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. John Jingu kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha Mbio za Wakili Marathon zilizofanyika Mei 31, 2026 Jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera (Katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Haki Mwanamke Mei 21, 2026 Jijini Dodoma