Upo Hapa: Home

MWAKYEMBE AKERWA NA RUSHWA

E-mail Print PDF

 

Na Bi. Farida Khalfan

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harisson Mwakyembe akerwa na vitendo vya rushwa katika sekta ya sheria.

Dkt. Mwakyembe aliyasema hayo, leo (05/01/2016) jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), amesema kuwa baadhi ya watendaji wa taaluma ya sheria sio waaminifu na hujihusisha na vitendo vya rushwa na hivyo kuharibu sifa ya taaluma ya sheria.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa vyombo vinavyosimamia sheria ndivyo vinavyoweza kuleta maendeleo nchini kwa kutenda haki kwa wananchi. Ameongeza, katika vyombo vya sheria kuna vijipu ambavyo viliachwa muda mrefu na kuwa majipu hivyo vianze kutumbuliwa kabla Rais Magufuli hajayatumbua.

Mbali na hayo Dkt. Mwakyembe amesema anafahamu changamoto zinazowakabili Mawakili wa Serikali ikiwemo usalama wao katika maeneo wanayoishi, amewasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii na atashirikiana nao kutatua changamoto zao.

Awali akizungumza kabla ya Kumkaribisha Waziri Mwakyembe, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Biswalo Mganga amesema ofisi yake katika kipindi cha mwaka jana (2015) imefanikiwa kukamata na kuchoma moto dawa za kulevya na kushinda kesi nane zinazohusu dawa hizo.

-Mwisho-

Matukio Mapya

Hakuna Tukio kwa sasa.

Anuani

KATIBU MKUU

  • Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria,
  • Barabara ya Mkalama,
  • Jengo la Taaluma Na. 1,
  • Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM,
  • S.L.B. 315,
  • DODOMA.
  • Simu:+255 26 2321680
  • Nukushi: +255 26 2321679
  • Tovuti www.sheria.go.tz
  • Barua pepe: km@sheria.go.tz