Upo Hapa: Home

SHERIA YA KULINDA MASHAHIDI NA WATOA TAARIFA ZA UHALIFU IMEANZA KUTUMIKA NCHINI

E-mail Print PDF

 

Sheria ya kulinda mashahidi na watoa taarifa za uhalifu nchini (The Whistleblower and Witness Protection Act. 2016) imeanza kutumika kuanzia tarehe 1 Julai, 2015. Sheria hiyo imekusudia kuweka mfumo wa kisheria utakaowezesha upatikanaji wa taarifa dhidi ya wahalifu wa makosa mbalimbali pasipo vikwazo na kulinda mashahidi na watoa taarifa hizo.

Kutumika kwa Sheria hiyo kunafuatia Tangazo la Serikali la tarehe 25 Machi, 2015 ambapo Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa sheria husika Dkt Harrison Mwakyembe ambaye aliidhinisha kuanza kutumika kwa sheria hiyo tarehe 1 Julai, 2016.

Taarifa za kuanza kutumika kwa Sheria hiyo zimetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utekelezaji Katiba Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Kamana Stanley alipokuwa akizungumza na wanahabari katika Ukumbi wa Idara ya Habari- MAELEZO.

Amesema kuwepo kwa sheria hii kutasaidia kuwapa ulinzi wa kisheria wale wote wanaotoa taarifa za uhalifu wa makosa ya aina mbalimbali wanayoshuhudia yakitendeka na kuongeza kuwa Sheria  hiyo itarahisisha utoaji na upatikanaji wa taarifa kwakuwa taarifa za uhalifu sasa zitatolewa na kupokelewa na vyombo vya dola,  vyombo vya habari na vyanzo vingine ambavyo Sheria hiyo imeviainisha.

“Uwepo wa Sheria hii utasaidia kuwapatia ulinzi wa kisheria wale wote wanaotoa taarifa za uhalifu wa makosa ya aina mbalimbali wanayoshuhudia yakitendeka na huku ikirahisisha utoaji na upatikanaji wa taarifa kwani taarifa za uhalifu sasa zitatolewa na pia kupokelewa si katika vyombo vya dola pekee bali pia kupitia vyombo vya habari na vyanzo vingine vinavyoainishwa katika sheria hiyo, alisema.

Amesema katika kufanikisha azma ya Serikali ya kupata tarifa dhidi ya uhalifu au ushahidi kwa wakati na uhakika inakamilika Sheria hiyo imeweka utaratibu wa namna ya kushughulika na wale wote watakaoshindwa kushughulikia vyema taarifa zinazotolewa kwao na kuruhusu watoa taarifa na mashahidi kupata madhara.

Pia amesema Sheria hiyo imemeweka utaratibu wa kupatiwa motisha ikiwa ni pamoja na kuwafidia wale ambao wataathirika kutokana na taarifa walizotoa. wale wote wanaofanikisha kuokoa mali ya umma, kupatikana kwa wahalifu, kulinda mazingira na maisha ya binadamu kutokana na uhalifu uliopangwa kufanyika lakini uhalifu huo kuzuiwa kutokana na taarifa iliyotolewa katika mamlaka husika.

Bwana Kamana ametoa wito kwa wananchi kujitokeza bila woga na kutoa taarifa za uhalifu dhidi ya matendo ya aina zote yanayofanywa kinyume cha sheria na hivyo kusaidia Serikali katika mapambano dhidi ya uhalifu na kujenga jamii na taifa linalopinga uhalifu.

Matukio Mapya

Hakuna Tukio kwa sasa.

Anuani

KATIBU MKUU

  • Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria,
  • Barabara ya Mkalama,
  • Jengo la Taaluma Na. 1,
  • Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM,
  • S.L.B. 315,
  • DODOMA.
  • Simu:+255 26 2321680
  • Nukushi: +255 26 2321679
  • Tovuti www.sheria.go.tz
  • Barua pepe: km@sheria.go.tz