Upo Hapa: Home

TUMEDHAMIRIA KUWASAJILI WATOTO WOTE NCHINI -WAZIRI MWAKYEMBE

E-mail Print PDF

 

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwasajili watoto wote nchini wenye umri chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa.

Dhamira hiyo ya Serikali inalengo la kuiondoa nchi katika takwimu zinazoonyesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwisho barani Afrika ambazo watoto hawana vyeti vya kuzaliwa.

Dkt Mwakyembe amesema hayo mjini iringa alipokuwa akizindua kampeni ya uandikishaji watoto chini ya miaka mitano katika mikoa ya Iringa na Mbeya iliyofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa.

Dkt Mwakyembe ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho cha kuwa miongoni mwa nchi ambazo watoto wake hawajasajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa na kusema kuwa ndio maana kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikaamua kuendesha kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano.

Amesema serikali imedhamiria kuiondoa Tanzania katika hali hiyo kwakuwa sio sahihi kwa nchi kuwa katika nafasi hiyo sawa na Somalia

'Hali hii sio sahihi, Tanzania haistahili kuwepo katika kundi hilo tumedhamiria kuiondoa nchi huko, tunataka Tanzania iwe juu ktk usajili wa watoto kama ilivyo juu kwa chanjo mbalimbali kwa watoto wetu' alisema.

Mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha watoto wote chini ya miaka mitano wanasajiliwa na kuwa ma vyeti vya kuzaliwa unaendeshwa kupitia Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi RITA chini ya ufadhili wa UNICEF. Ends

Pichani Waziri wa Mambo ya Katiba na sheria Dkt Harrison Mwakybe akikata utepe kuzindua kampeni maalum ya kuwasajili wayoto chini ya miaka mitano nankuwapatoa vyeti vya kuzaliwa katika mikoa ya Iringana Njombe iliyofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa

-Mwisho-

 

Matukio Mapya

Hakuna Tukio kwa sasa.

Anuani

KATIBU MKUU

  • Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria,
  • Barabara ya Mkalama,
  • Jengo la Taaluma Na. 1,
  • Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM,
  • S.L.B. 315,
  • DODOMA.
  • Simu:+255 26 2321680
  • Nukushi: +255 26 2321679
  • Tovuti www.sheria.go.tz
  • Barua pepe: km@sheria.go.tz