Upo Hapa: Home

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UPR AFRIKA

E-mail Print PDF

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UPR AFRIKA

 

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango na kuzungumza jinsi ya kusaidia utekelezaji wa mapendekezo 130 ambayo Serikali iliyakubali mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitia Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu.Mhe. Waziri Mwakyembe amesema Serikali kama ambavyo ilivyoridhia mapendekezo hayo itasimama imara kuhakikisha yanatekelezwa kikamilifu na hivyo kuimarisha hali ya haki za binadamu nchini.

Amesema nia ya Serikali ni kuona haki za bindamu nchini zinaheshimiwa  bila ya kuingilia au kukiuka  mila, tamaduni , desturi na imani za kidini ambazo Tanzania imekuwa ikizifuata au kuziamini tangu enzi.

Nae bw. Onyango alisema kwamba wao kama taasisi isiyo ya kiserikali wanafanya kazi na serikali mbalimbali duniani, taasisi zisizo za serikali na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha haki za binadamu zinaimarishwa na kuthaminiwa na kuongeza kuwa lengo hasa la kukutana kwake ni kujitambulisha na kuomba kufanya kazi na serikali katika kuhakikisha mapendekezo yaliyokubaliwa yanatekelezwa kikamailifu.

Pia aliomba kupatiwa nafasi ya kutoa mafunzo jinsi ya utekelezaji huo kwa taasisi na watumishi wa umma wanaohusika na utekelezaji wa mapendekezo hayo ili kufanikisha mpango wa utekelezaji wa mapendekezo hayo.

Alisema kwamba lengo lao kuu  ni kuunganisha mpango wa tathmini ya hali ya haki za binadamu nchini ili uendane na mpango wa malengo ya milenia ili kuweza kufikia maendeleo ya kweli huku haki za binadamu zikiimarishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Mwezi Septemba 2016, Serikali iliyakataa mapendekezo 94, kuyaangalia upya mapendekezo 25 na kukubali 130 kati ya 227 yaliyotolewa na mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa, likiwemo suala la hali ya kisiasa Zanzibar. Tamko hilo lilitolewa kwenye mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitisha Ripoti ya Tathmini ya Dunia (UPR) mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitia Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu kwa nchi wanachama uliofanyika mjini Geneva nchini Uswisi..

Matukio Mapya

Hakuna Tukio kwa sasa.

Anuani

KATIBU MKUU

  • Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria,
  • Barabara ya Mkalama,
  • Jengo la Taaluma Na. 1,
  • Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM,
  • S.L.B. 315,
  • DODOMA.
  • Simu:+255 26 2321680
  • Nukushi: +255 26 2321679
  • Tovuti www.sheria.go.tz
  • Barua pepe: km@sheria.go.tz