Upo Hapa: Home

Mtanzania Felistas Joseph, achaguliwa kuongoza Kamati ya nchi za Maziwa Makuu ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari

E-mail Print PDF

Mtanzania Felistas Joseph, amechaguliwa kuongoza Kamati ya nchi za Maziwa Makuu ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari (International Conference on Great Lakes Region –ICGLR).

 

Bibi Felistas amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo katika uchaguzi uliofanyika mjini Pointre Noire, nchini Congo Desemba Mosi mwaka 2016. Kamati iliyoundwa chini ya Itifaki ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari inajumuisha wajumbe 12 kutoka nchi wanachama wa ICGLR  ambapo wajumbe hao huidhinishwa na Baraza la Mawaziri la ICGLR (Regional Inter-Ministerial Council- RIMC).

 

Bibi Felistas ni Mkurugenzi  Msaidizi  katika Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria na amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Tanzania ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari tangu ilipoundwa mwezi Februari mwaka 2012.

 

Katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanda, Bibi Felistas atasaidiwa na Makamu Mwenyekiti kutoka nchini Burundi, Katibu kutoka DRC ambao kwa pamoja wanatarajiwa kuthibitishwa na Baraza la Mawaziri la ICGLR  katika kikao chao kitakachofanyika wiki mbili  zijazo nchini Kenya.

Matukio Mapya

Hakuna Tukio kwa sasa.

Anuani

KATIBU MKUU

  • Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria,
  • Barabara ya Mkalama,
  • Jengo la Taaluma Na. 1,
  • Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM,
  • S.L.B. 315,
  • DODOMA.
  • Simu:+255 26 2321680
  • Nukushi: +255 26 2321679
  • Tovuti www.sheria.go.tz
  • Barua pepe: km@sheria.go.tz