Upo Hapa: Home

WATUMISHI WIZARA YA KATIBA NA SHERIA WAKUTANA KUJADILI SHERIA YA NDOA NA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA

E-mail Print PDF

WATUMISHI WIZARA YA KATIBA NA SHERIA WAKUTANA KUJADILI SHERIA YA NDOA NA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria wamekutana kupitia na kujadili mapendekezo ya kuboresha Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na Muswada wa kutunga Sheria ya Msaada wa Huduma za Sheria ambao ulisomwa Bungeni mara ya kwanza katika bunge lililopita.

Kusanyiko hilo la watumishi hao wa wizara limefanyika katika ukumbi wa mikutano wizarani na kuongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju ambaye alitumia nafasi hiyo kuwasisitizia watumishi kuzingatia Sera, Sheria, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma ili kutoa huduma bora kwa wananchi ambao wanawahudumia.

Kikao hicho kimefanyika ili kuwapa nafasi watumishi hao wa wizara kujua yanayoendelea na kutoa mapendekezo ya maboresho juu ya Sheria hizo mbili ambayo yanaendelea kupitia  wadau mbalimbali na hivyo kupata Sheria ya Huduma ya Msaada wa Sheria na kuboresha Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 ili iendane na matakwa ya wananchi na wakati.

Katika kikao hicho pia wataumishi wa wizara walipata fursa ya kuuliza masuala mbalimbali juu ya sheria hizo mbili  pamoja na mambo mengine yanayowahusu watumishi  ambayo Mkurugenzi wa Utawala Bw Aloyce Mwagofi alikuwapo na kuwafafanulia.

Matukio Mapya

Hakuna Tukio kwa sasa.

Anuani

KATIBU MKUU

  • Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria,
  • Barabara ya Mkalama,
  • Jengo la Taaluma Na. 1,
  • Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM,
  • S.L.B. 315,
  • DODOMA.
  • Simu:+255 26 2321680
  • Nukushi: +255 26 2321679
  • Tovuti www.sheria.go.tz
  • Barua pepe: km@sheria.go.tz