Upo Hapa: Home

WATUMISHI WA UMMA WAASWA KUFANYA KAZI KWA MAADILI NA WELEDI

E-mail Print PDF

 

Watumishi wa Umma wametakiwa kufanya kazi kwa maadili na weledi katika kipindi chote cha utumishi wa umma.

Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo.

Bwana Mbonde alisema kuwa watumishi wa umma wanatakiwa muda wote kufanya kazi kwa maadili na weledi ikiwa na kutojihusisha na vitendo vya ufisadi.

Alisema kuwa watumishi wengi wa umma kutokana na kushindwa kufuata maadili ya utumishi wa umma, wamejikuta wakijiingiza katika vitendo vya rushwa na ufisadi hivyo kupelekea utendaji wao wa kazi kuwa duni na hatimaye kutofikia malengo Wizara yaliyopangwa.

Katibu Mkuu huyo aliwataka pia viongozi wa Wizara kuwaheshimu walio chini yao kwa kutenda haki na kuheshimu kazi zao kila mmoja katika daraja lake alilonalo ili kuongeza ari na ufanisi zaidi katika utendaji kazi.

Aidha, amewataka watumishi hao kudumisha umoja, mshikamano na amani kwa kuacha tabia za chuki miongoni mwa watumishi ambazo zinapelekea kuwepo kwa makundi yanayorudisha nyuma utendaji wa kazi.

Aliwaasa watumishi hao kusoma maandiko matakatifu ambayo ndiyo nguzo muhimu katika maisha kwa kusamehe na kutohesabu makosa mara kunapotokea makwazo katika utendaji wa kazi.

Pia aliwataka watumishi wa umma kuwa na uvumilivu mkubwa katika kazi kwa vile utumishi wa umma ni safari ndefu inayohitaji weledi mkubwa na uadilifu uliojikita katika kanuni na taratibu za utawala bora katika utendaji kazi.


Bw. Mbonde  ni mtumishi wa umma  ambaye ametumikia kazi muda wa miaka 60 na kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyadhifa ya Katibu Mkuu ambayo ndiyo ameitumikia kwa miaka miwili katika Wizara ya Katiba na Sheria hadi kustaafu kwake August 13, 2014.


Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Moses Chitama aliyewakilisha watumishi wa Wizara  amempongeza  Katibu Mkuu huyo kwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa katika muda wote wa utumishi wa Umma.

Alisema utumishi wa Katibu Mkuu huyo msataafu ni wa kuigwa kwa kuwa alikuwa ni kiongozi mcha Mungu, mwenye maadili, mpole, mnyenyekevu na mpenda haki ambaye hakupenda kuona mtumishi yeyote ananyanyasika katika utendaji wake wa kazi.   

-Mwisho-

 

Matukio Mapya

Hakuna Tukio kwa sasa.

Anuani

KATIBU MKUU

  • Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria,
  • Barabara ya Mkalama,
  • Jengo la Taaluma Na. 1,
  • Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM,
  • S.L.B. 315,
  • DODOMA.
  • Simu:+255 26 2321680
  • Nukushi: +255 26 2321679
  • Tovuti www.sheria.go.tz
  • Barua pepe: km@sheria.go.tz